array(0) { } Radio Maisha | Polisi Kaunti ya Busia wamkamata mwanamume anayedaiwa kumuuma mkewe mdomo na sikio

Polisi Kaunti ya Busia wamkamata mwanamume anayedaiwa kumuuma mkewe mdomo na sikio

Polisi Kaunti ya Busia wamkamata mwanamume anayedaiwa kumuuma mkewe mdomo na sikio

Maafisa wa Polisi katika Kaunti ya Busia, wamemtia nguvuni mwanamume anayedaiwa kumuuma mdomo na sikio mke wake kufuatia mzozo kati yao katika eneo la Nambale.

OCPD wa Nambale, Robert Ndambiri, amesema mshukiwa Pascal Omusungu ambaye alikuwa amekwenda mafichoni baada ya  tukio hilo ametiwa mbaroni mapema leo asubuhi alipokuwa katika shamba la miwa  karibu na boma lake.

Ndambiri amesema Omusungu mwenye umri wa miaka hamsini na moja alinaswa kufuatia taarifa kutoka kwa umma na anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Nambale akisubiri kufikishwa kesho mahakamani na kushtakiwa

Hapo jana mwanamume huyo alimshambuliwa mkewe Jackline Kerubo mwenye umri wa miaka 39, baada ya kumpa jirani yake mboga hata baada ya mumewe kumwonya kutofanya hivyo.

Kerubo, ambaye ameolewa na jamaa huyo kwa miaka 21 ,amesema mshukiwa alimshambuliwa akiwa jikoni kabla ya kumuuma mdomo wa chini na sikio.