array(0) { } Radio Maisha | Ngilu amshtaki spika wa Bunge la Kitui kuhusu matumizi ya fedha

Ngilu amshtaki spika wa Bunge la Kitui kuhusu matumizi ya fedha

Ngilu amshtaki spika wa Bunge la Kitui kuhusu matumizi ya fedha

Gavana wa Kitui, Charity Ngilu amewasilisha kesi kutaka mahakama kumshurutisha Spika wa Bunge la Kitui, George Mutua kumruhusu azitumie fedha zilizotengewa serikali yake.

Ngilu amewasilisha kesi hiyo baada ya Mhasibu Mkuu wa Serikali kumwandikia barua Waziri wa Fedha wa kaunti hiyo kwamba pesa hizo zinaweza kutolewa tu baada ya Spika kutia saini.

Bunge la kaunti hiyo lilipitisha bajeti ya mwaka huu wa kifedha mnamo Juni 28 mwaka huu ila Spika hajatia saini wala kuizungumzia bajeti yenyewe.

Ngilu anasema hatua ya spika huyo kutoidhinisha bajeti hiyo imehujumu utendakazi katika serikali yake hali ambayo imechangia pakubwa kukwama kwa miradi ya maendeleo.