array(0) { } Radio Maisha | Wakazi wa Pangani wakadiria hasara baada ya nyumba zao kubomolewa

Wakazi wa Pangani wakadiria hasara baada ya nyumba zao kubomolewa

Wakazi wa Pangani wakadiria hasara baada ya nyumba zao kubomolewa
 

Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Pangani, kwenye Kaunti ya Nairobi wamekesha nje baada ya matingatinga ya Serikali ya Kaunti kubomoa nyumba zao na kuwafurusha.

Kwa mujibu wa mmoja wa wakazi hao, matingatinga hayo yaliwasili mwendo wa saa tano unusu usiku wa kuamkia leo kabla ya kuanza ubomoaji huo na hivyo kuwalazimu kutorokea usalama.

Ikumbukwe kuwa mtaa huo ni miongoni mwa mingine saba kwenye Kaunti ya Nairobi ambayo serikali ya kaunti inalenga kupandisha hadhi kwa kukarabatitwa upya. Mitaa mingine ni Uhuru, New Ngara, Old Ngara, Suna Rad, Ngong Road 1 na 2 pamoja na Jeevanjee.