array(0) { } Radio Maisha | Wakenya washauriwa kujitokeza kwa shughuli ya sensa mwezi ujao

Wakenya washauriwa kujitokeza kwa shughuli ya sensa mwezi ujao

Wakenya washauriwa kujitokeza kwa shughuli ya sensa mwezi ujao

Baraza la Maimamu, SUPKEM limetoa wito kwa Wakenya kujitokeza ili kushiriki shughuli ya sensa itakayoanza mwezi ujao.

Naibu Katibu Mkuu wa baraza hilo Washalla Abdhi amesema hatua hiyo itatoa mwelekeo kwa serikali kuu kuhusiana na mpangilio wa kutoa huduma bora kwa raia wake.

Aidha Washalla amewashauri Wakenya wanaoishi mijini kurejea maeneo walikozaliwa ili kuhesabiwa kwa lengo la kuziwezesha kaunti zao kupata fedha za kutosha za maendeleo wakati wa uundaji wa bajeti.
 

Shughuli hiyo itaanza tarehe 24 mwezi Agosti na kukamilika tarehe 31 mwezi uo huo.