array(0) { } Radio Maisha | Mataifa zaidi kukabidhiwa ardhi ya kujenga bandari kavu

Mataifa zaidi kukabidhiwa ardhi ya kujenga bandari kavu

Mataifa zaidi kukabidhiwa ardhi ya kujenga bandari kavu

Jumla ya mataifa matano yanatarajiwa kukabidhiwa ardhi katika eneo la Naivasha ili kujenga Bandari ya Nchi Kavu. Tayari Rais Kenyatta ameyaahidi mataifa ya  Uganda na Sudan Kusini kufuatia ziara za  Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir.

Kenya inalenga mataifa mengine yote Afrika Mashariki isipokuwa Tanzania ambayo Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambayo hayana bandari zao hivyo kutegemea bandari za Tanzania na Kenya.

Tayari mabwawa manne yamechimbwa ili kutosheleza mahitaji ya maji huku kwa jumla shilingi milioni 700 zikitengwa kwa huduma za maji . Serikali inalenga kujenga eneo la viwandani  karibu na kituo cha Reli ya Kisasa SGR miongoni mwa hatua nyingine za kuboresha utendakazi wa huduma za bandari.