array(0) { } Radio Maisha | Watu zaidi watarajiwa kufurushwa kutoka Msitu wa Mau
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu zaidi watarajiwa kufurushwa kutoka Msitu wa Mau

Watu zaidi watarajiwa kufurushwa kutoka Msitu wa Mau

Mvutano mwingine kati ya serikali na wakazi wa Msitu wa Mau unatarajiwa hivi karibuni baada ya serikali kutangaza awamu ya pili ya kuwafurusha waliobadili msitu huo kuwa makazi yao.

Waziri wa Mazingira Keriako Tobiko amesema kuwa shughuli hiyo itang'oa nanga hivi karibuni huku akisisitiza kwamba hakuna atakayefidiwa kwani wanaoishi katika msitu huyo walinyakuwa ardhi ya serikali.

Aidh, Tobiko amedokeza kwamba kufikia sasa, serikali imerejesha ekari elfu kumi na moja za ardhi zilizokuwa zimetwaliwa na jamii zinazoishi kwenye msitu huo. Tobiko ambaye alikuwa ameandamana na mwenzake wa Ugatuzi Eugene Wamalwa katika hafla iliyoandaliwa kwenye Kaunti ya Narok, amesema kwamba hatua za kuuhifadhi msitu huo inaungwa mkono kikamilifu na Baraza zima la Mawaziri.

Wakati uo huo, Waziri huyo amepuuza taarifa kwamba wapo baadhi ya wakaazi walio na hati miliki za ardhi akisema kwamba hati hizo zilipatikana kwa njia za mkato huku akiapa kutotishika na matamshi ya wanasiasa wa eneo hilo ambao wamekuwa wakipinga kufurushwa huko kwa kujitaftia umaarufu wa kisiasa.