array(0) { } Radio Maisha | Jopo la maridhiano BBI limepinga vikali madai kwamba limewasilisha ripoti kwa Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM, Raila Odinga

Jopo la maridhiano BBI limepinga vikali madai kwamba limewasilisha ripoti kwa Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM, Raila Odinga

Jopo la maridhiano BBI limepinga vikali madai kwamba limewasilisha ripoti kwa Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM, Raila Odinga

Jopo lililobuniwa kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kufuatia mwafaka wa mwezi Machi baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga limepinga vikali madai kwamba limewasilisha ripoti kwa Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM, Raila Odinga.

Jopo hilo likiongozwa na Mwenyekiti wake, Yussuf Haji ambaye pia ni Seneta wa Garissa limetaja madai hayo kuwa yasiyokuwa ya kweli, na kwamba wangali wanakusanya maoni ya Wakenya.

Kwa mujibu wa Haji, jopo hilo halijaandaa ripoti yoyote wala kuwasilisha baadhi ya mapendekezo kwa viongozi hao.

Miongoni mwa mapendekezo ambayo yanadaiwa kuyawasilisha kwa Rais Kenyatta na Raila Odinga, ni kwamba Rais wa taifa hili ataongoza kwa muhula wa mwaka mmoja wa miaka saba, kuwapo kwa wadhifa wa Waziri mkuu na kujumuishwa kwa serikali za mikoa kumi na nne.

Aidha inadaiwa kwamba ripoti hiyo, ilipendekeza mawaziri wasiozidi ishirini wateuliwe miongoni mwa wabunge, ikiwa ni pamoja na manaibu waziri mkuu wawili.

Hata hivyo kwenye kikao na wanahabari  Jijini Nairobi, Haji amepinga madai hayo akisema Jopo hilo bado halijamaliza kutembelea kaunti zote, ili kuchukua maoni ya wananchi.

Jopo hilo linatarajiwa kutembelea kaunti za Kwale na Lamu Jumanne kabla ya kuelekea Trans Nzoia, Bungoma , Taita Taveta , na hatimaye Kaunti ya Pokot Magharibi, kwani tayari limechukua maoni kwenye kaunti 39.

Ikumbukwe jana, baadhi ya viongozi katika Chama cha Jubilee walihusisha Jopo hilo , makundi ya Embrace Kenya na Kieleweke kuwa njama ya Kinara wa ODM Raila Odinga kutaka kuhujumu umoja wa chama hicho.