array(0) { } Radio Maisha | Baraza la Magavana leo limewasilisha kesi mahakamani kufuatia mgogoro wa Ugavi wa Mapato wa Mwaka 2019/ 20

Baraza la Magavana leo limewasilisha kesi mahakamani kufuatia mgogoro wa Ugavi wa Mapato wa Mwaka 2019/ 20

Baraza la Magavana leo limewasilisha kesi mahakamani kufuatia mgogoro wa Ugavi wa Mapato wa Mwaka 2019/ 20

Baraza la Magavana leo limewasilisha kesi katika Mahakama ya Juu kufuatia mgogoro wa Ugavi wa Mapato wa Mwaka 2019/ 20 kwa karani wa Mahakama ya Juu kabla ya kuelekea katika Jengo la KICC ambako wamekutana na wawakilishi wa mashirika ya kijamii, lengo kuu likiwa kushinikiza kutengewa fedha wanazoidai serikali kuu kupitia Mswada huo wa Ugavi wa Mapato. Rosa Agutu anakamilisha taarifa hii.

 

Mgogoro kati ya Bunge la Kitaifa na lile Seneti ulianza wakati ambapo Bunge la Kitaifa lilipopitisha bajeti ya shilingi bilioni 310 huku Bunge la Seneti kwa ushirikianao na Baraza la Magavana likipitisha bajeti yashilingi bilioni 335 kisha kupunguza hadi bilioni 327.

Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Wycliffe Oparanya amesema kukosa kutolewa kwa fedha za kuendesha serikali za kaunti ni ishara tosha kuwa serikali kuu inalenga kulemaza ugatuzi.

 

Gavana wa Kisumu Anyang' Nyong'o kwa upande wake amesema kuwa shughuli za kaunti zimesitishwa kufuatia kutopitishwa kwa bajeti hiyo na kusema kuwa wanaoumia mabunge hayo mawili yakiwa na mgogoro ni wanachi.

 

Kwa mujibu wa rufaa hiyo, maseneta vilevile wanataka ufafanuzi kuhusu miswada 21 iliyopitishwa katika Bunge la Kitaifa pasi na kuhusishwa kwa Bunge la Seneti.

Hata hivyo maseneta hawakuwa katika maandamano hayo isipokuwa Seneta wa Kakamega, Cleophas Malala ambaye aliwatetea maseneta wenzake akisema kuwa wenzake hawakukwepa maandamano hayo kwani wanaungana na magavana katika uwasilishaji wa rufaa hiyo.

 

Seneta wa pili aliyefika katika jengo la Mahakama ya Juu baada ya maandamano hayo ni wa Siaya James Orengo ambaye alisema walifanya kikao na magavana siku chache zilizopita hivyo wameafikiana na kusisitiza kuwa ugatuzi ndio msingi wa katiba.

 

Ikumbukwe kuwa mabunge hayo mawili yamekuwa yakivutana kuhusu kiwango cha fedha zinazofaa kutengewa magatuzi. Kesi hiyo itasikilizwa siku ya Ijumaa wiki hii.