array(0) { } Radio Maisha | Magavana kuandamana kuhusu Mswada wa Ugavi wa Mapato wa Mwaka 2019/20
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Magavana kuandamana kuhusu Mswada wa Ugavi wa Mapato wa Mwaka 2019/20

Magavana kuandamana kuhusu Mswada wa Ugavi wa Mapato wa Mwaka 2019/20

 

Magavana chini ya mwamvuli wa Baraza la Magavana wanatarajiwa kuandamana kutoka Hoteli ya Intercontinental kuelekea katika Mahakama ya Juu watakakowasilisha kesi kuhusu Mswada wa Ugavi wa Mapato wa Mwaka 2019/20.

Baadae baraza hilo ambalo linatarajiwa kuandamana na maseneta na Wawakilishi Wadi, litaelekea katika Jengo la KICC ambako watakutana na wawakilishi wa mashirika ya kijamii, lengo kuu likiwa kushinikiza kutengewa kwa fedha wanazodai na serikali kuu kupitia Mswada huo wa Ugavi wa Mapato. Wylcif Wangamati ni Gavana wa Bungoma.

 

Kwa mujibu wa Seneta wa Nandi, Samson Cherargei mbali na suala la ugavi wa mapato, maseneta pia watakuwa wakitaka ufafanuzi kuhusu miswada 21 iliyopitishwa katika Bunge la Kitaifa pasi na kuhusishwa kwa Bunge la Seneti. Ikumbukwe kuwa tayari Naibu wa Rais, William Ruto aliwashauri magavana na maseneta kutoelekea mahakamani na badala yake kuzungumza.

Haya yanajiri wakati ambapo mabunge hayo mawili yamekuwa yakivutana kuhusu kiwango cha fedha zinazofaa kutengewa magatuzi baada ya wabunge kushikilia pendekezo la shilingi bilioni 316 na maseneta kupendekeza bilioni 327 hali ambayo haijaafikiwa kufikia sasa. Aden Duale ni Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa.