array(0) { } Radio Maisha | Madereva wa Taxi jijini Nairobi wameanza mgomo

Madereva wa Taxi jijini Nairobi wameanza mgomo

Madereva wa Taxi jijini Nairobi wameanza mgomo

Madereva walioko katika muungano wa Digital Taxi Forum wanaohudumu jijini Nairobi, wameanza mgomo asubuhi hii kulalamikia kutotekelezwa kwa mkataba wa maelewano kati yao na kampuni za wahudumu wa texi uliotiwa saini mwaka 2017.

Miongoni mwa masuala wanayolalamikia ni kutoongezwa kwa viwango vya nauli wanavyostahili kuwatoza wateja jijini Nairobi, hali ambayo inachangia mapato duni kwao ikizingatiwa viwango vya matozo katika miji mingine mfano Mombasa na Kisumu ni vya juu.

Madereva hao wanasema wakati umewadia kwa serikali kuzidhibiti kampuni za Uber, Taxify na nyingine ambazo wamiliki wake ni raia wa mataifa ya nje, akisema zinawahujumu madereva humu nchini kwa kuwawekea sheria bila kushauriana nao.