array(0) { } Radio Maisha | Raia Kumi na wanane kutoka Ethiopia wakamatwa Moyale.

Raia Kumi na wanane kutoka Ethiopia wakamatwa Moyale.

Raia Kumi na wanane kutoka Ethiopia wakamatwa Moyale.

Maafisa wa polisi wanaendelea kuwazuilia watu kumi na wanane waliokamatwa jana jioni wakija jijini Nairobi kutoka Moyale nchuini Ethiopia.

Inaarifiwa kuwa tisa miongoni mwao ni raia wa Ethiopia, saba wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na ambao ni watoto wadogo. Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali raia saba wa Kongo walikuwa wametoroka kutoka kambi ya wakimbizi nchini Uganda.

Haya yakijiri, raia wanne wa Eritrea wenye umri wa miaka kati ya 20 na 25 wanazuiliwa katika kituo kimoja cha Polisi kwenye Kaunti ya Marsabit baada ya kunaswa wakiwa nchini kinyume na sheria katika eneo la Turbi - Marsabit Kaskazini.