array(0) { } Radio Maisha | Pesa zenu ziko salama.
Pesa zenu ziko salama.

Pesa zenu ziko salama, ndiyo taarifa ya kampuni za michezo ya bahati nasibu kwa wateja wao.

Katika tarifa kwa vyombo vya habari, kapuni hizo zikiongozwa na Kampuni za SportPesa na Betin Kenya, zimewahakikisha wateja wao ambao hawakuweza kuzitoa fedha zao wakati wa muda wa makataa ya saa arubaini na nane uliotolewa na serikali kwamba watazipata fedha hizo.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa kampuni hizo ni kwamba, mazungumzo yanaendelea kati yao na serikali vilevile Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi, KRA ili kupata mwafaka.

Ikumbukwe Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiang'i aliagiza Kampuni ya Mawasiliano, Safaricom kuzifunga laini ambazo hutumika kuweka na kutoa fedha za kamari, yaani Paybill number za kampuni 27.

Kufikia jana, SportPesa na Betin Kenya zilitangaza kwamba watu zaidi ya elfu moja huenda wakapoteza ajira kufuatia hatua ya serikali kuzifunga kampuni hizo.