array(0) { } Radio Maisha | Magavana kushinikiza serikali kuu ili kutengewa fedha zaidi.

Magavana kushinikiza serikali kuu ili kutengewa fedha zaidi.

Magavana kushinikiza serikali kuu ili kutengewa fedha zaidi.

Baraza la Magavana sasa linafanya mikakati ya mwisho kabla ya kuanza mchakato wa kushinikiza kutengewa fedha wanazodai na serikali kuu kupitia Mswada wa Ugavi wa Mapato.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti, Wyclif Oparanya kuanzia kesho magavana watachuka harakati kadhaa zikiwamo kuelekea mahakamani na hata kuandamana  nje ya Ofisi za Wizara ya Fedha. Magavana wanatarajiwa kuungwa mkono na Maseneta na Wawakilishi Wadi.

Kwa mujibu wa Seneta wa Nandi, Samson Cherargei mbali na Suala la ugavi wa mapato, maseneta pia watakuwa akitaka ufafanuzi kuhusu miswada 21 iliyopitishwa katika Bunge la Kitaifa pasi na kuhusishwa kwa Bunge la Seneti.  Jana, Naibu wa Rais, William Ruto aliwashauri magavana na maseneta kutoelekea mahakamani na badala yake kuzungumza.

 

Wakati uo huo  Mbunge wa Mwingi ya Kati Dkt Gedion Mulyungi ameunga mkono pendekezo la Spika wa Bunge  la Seneti Ken Lusaka la kutaka Bunge la Kitaifa na seneti kuafikiana kuhusu Mswada wa Ugavi wa Mapato.

 

 

Akizungumza wakati wa ziara  katika Shule ya Msingi ya Nguni Mulyungi amesema tofauti baina ya mabunge hayo mawili zitaathiri utendakazi wa serikali na hivyo kuwa kikwazo katika miradi ya maendeleo nchini.

 

Mulyungi vilevile amesema mabunge hayo mawili yanafaa kuhakikisha yanatekeleza majukumu yake ipasavyo kisheria kwa kuangazia maslahi ya Wakenya badala ya kushiriki mabishano.

Haya yanajiri wakati ambapo mabunge hayo mawili yamekuwa yakivutana kuhusu kiwango cha fedha zinazofaa kuitengewa magatuzi baada ya wabunge kushikilia pendekezo la shilingi bilioni 316 na maseneta