array(0) { } Radio Maisha | matrekta za kampuni ya sukari yatikiwa kufuata sheria za trafik

matrekta za kampuni ya sukari yatikiwa kufuata sheria za trafik

matrekta za kampuni ya sukari yatikiwa kufuata sheria za trafik

Kampuni za Sukari kwa mara nyingine tena zimetakiwa kuhakikisha kuwa matrekta yanayotumika kusafirisha miwa yanaafiki sheria za trafiki kabla ya kuruhusiwa kuhudumu barabarani.

Wito huu umejiri baada ya visa vya matrekta kuwagonga watu kuongezeka katika barabara ya Bukembe - Nzoia huku kisa cha hivi karibuni kikiwahusisha watu wawili.

Ndicho kilio cha wakazi wa eneo hili ambao wamezitaka kampuni za kutengeneza sukari kuhakikisha madereva wa matreka yao wanazingatia sheria za barabarani.

Anthony Juma ambaye ni mhudumu wa Bodaboda kwenye barabara ya Bukembe - Nzoia, amesema baadhi ya Matrekta hayo huendeshwa kwa kasi hata wakati wa usiku licha ya kutokuwa na taa za kumulika gizani.

Aidha amesema matrekta hayo yanaposababisha kifo cha mtu kwenye ajali, huzuiliwa kwa muda mfupi tu katika Vituo vya Polisi kisha kuachiliwa hata bila uchunguzi kufanyika.

Kauli sawa na hiyo imetolewa na Kevin Nyongesa ambaye ni Mwenyekiti wa wanabodaboda katika eneo hilo huku akisisitiza kuwa baadhi ya Matrekta hayo huharibikia njiani na kuegeshwa bila kuwekwa ishara ya ajali kwa watumiaji wengine wa barabara hivyo kusababisha ajali.

Katika barabara hiyo ya Bukembe - Nzoia, kumeshuhudia ajali mbili zilizosababisha vifo vya watu wawili katika muda usiozidi Miezi miwili kisa cha hivi punde kikiwa cha kijana aliyezikwa jana Jumamosi.

Kutokana na hali hiyo Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa ametaka kampuni husika kuwajibika ili kupunguza visa vya ajali zinazosababishwa na matrekta hayo.