array(0) { } Radio Maisha | mwanamume mmoja avamiwa na ndovu Meru.

mwanamume mmoja avamiwa na ndovu Meru.

mwanamume mmoja avamiwa na ndovu Meru.

Huenda mzozo kati ya binadamu na ndovu katika kaunti ya Meru ukachukua mkondo mwingine iwapo Shirika la Huduma za Wanyamapori KWS halitaweka mikakati ya kukabili mgogoro huo.

Hali hii inajiri wakati ambapo mwanamume mwenye umri wa miaka 43 amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na ndovu watatu katika kijiji cha Ndunyuruma kwenye kaunti hiyo.

Jonadhan Baariu alikuwa shambani akifanya shughuli zake za ukulima kabla ya ndovu hao kumvamia kutoka msituni unaopakana na shamba alake.

Jonathan amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Isiolo ambapo ameelezea jinsi alivyovamiwa na ndovu hao baada ya kujificha alipowaona.

Naibu Chifu wa eneo la Kithima Paul Muriira amesema ndovu hao wamekuwa wakiwavamia na kuwajeruhi wakazi wa eneo hilo kutoka katika Hifadhi ya Wanyamapori ya Isiolo huku akiwasihi maafisa wa Shirika la KWS kuingilia kati suala hilo kwani hali hiyo inahatararisha maisha ya binadamu.