array(0) { } Radio Maisha | Watu kadhaa wauliwa katika shambulio la kigaidi nchini Somalia

Watu kadhaa wauliwa katika shambulio la kigaidi nchini Somalia

Watu kadhaa wauliwa katika shambulio la kigaidi nchini Somalia

Raia watatu wa Kenya ni miongoni mwa watu ishirini na sita ambao wameripotiwa kuuliwa nchini Somalia katika shambulio la kigaidi kwenye hoteli moja mjini Kismayu. Kwa mujibu wa rais wa jimbo la Jubaland, Ahmed Madobe, wengine waliouliwa ni raia watatu wa Tanzania, wawili wa Marekani, mmoja wa Uingereza na mwingijne mmoja wa Canada.

Watu wengine hamsini na sita wamejeruhiwa katika shambulio hilo lililotekelezwa na  washambulizi wa kundi la kigaidi la Al Shabaab ambao tayari wamekiri kuhusika. Mwanahabari tajika nchini Somalia kwa jina Hodan Naleyah na mumewe vilevile wameuliwa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi nchini humo, Meja Mohamed Abdi, watu kadhaa waliokolewa wakati wa shambulio hilo huku wavamizi wanne waliohusika wakiuliwa.

Wavamizi hao walikuwa wameivamia hoteli hiyo wakiwa na gari lililokuwa na vilipuzi huku wakiwalenga viongozi waliokuwa wakihudhuria mkutano wa kujadili masuala ya uchaguzi.