array(0) { } Radio Maisha | Watu wanne wafikishwa mahakani kwa tuhuma za mauaji.

Watu wanne wafikishwa mahakani kwa tuhuma za mauaji.

Watu wanne wafikishwa mahakani kwa tuhuma za mauaji.

Washukiwa wanne wa mauaji ya watoto wawili waliokamatwa katika Kijiji cha Keberesi  -Kenyenya Kaunti ya Kisii wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Ogembo, Gloria Barasa.

Afisa Mkuu wa Idara ya Upelelezi katika eneo la Kenyenya, Nicholus Wambugu ameiambia Mahakama ya Kisii kuwa wanne hao David Omwenga, Timothy Mainga, Gilbert Nyabuto na Evans Nyabuto walipatikana na shilingi elfu ishirini ZILIZOIBWA kutoka nyumba ya mwathiriwa.

Upande wa mashtaka aidha umeomba mahakama kuwazuilia wanne hao kwa siku kumi na nne zaidi katika Kituo cha Polisi cha Kenyenya ili kuruhusu uchunguzi. Kesi hiyo itatajwa tarehe mosi Agosti mwaka huu.

Baba wa watoto hao ameeleza jinsi alivyowakuta wanawe wakiwa wamenyongwa na kutupwa nje ya nyumba yao baada ya kutoka shuleni.