array(0) { } Radio Maisha | Madereva kufanya mgomo jijini Nairobi.

Madereva kufanya mgomo jijini Nairobi.

Madereva kufanya mgomo jijini Nairobi.

Madereva walioko katika muungano wa Digital Taxi Forum wanaohudumu jijini Nairobi, wanatarajiwa kufanya mgomo siku ya Jumatatu wiki ijayo kulalamikia kutotekelezwa kwa mkataba wa maelewano kati yao na kampuni za wahudumu wa texi uliotiwa saini mwaka 2017.

Kwa mujibu wa Wyclif Alutalala ambaye ni katibu wa muungano huo, miongoni mwa masuala wanayolalamikia ni kutoongezwa kwa viwango vya nauli wanavyostahili kuwatoza wateja jijini Nairobi, hali ambayo inachangia mapato duni kwao ikizingatiwa viwango vya matozo katika miji mingine mfano Mombasa na Kisumu ni vya juu.


Alutalala aidha amesema wakati umewadia kwa serikali kuzidhibiti kampuni za uber, taxify na nyingine ambazo wamiliki wake ni raia wa mataifa ya nje, akisema zinawahujumu madereva humu nchini kwa kuwawekea sheria bila kushauriana nao.

Wameahidi kugoma kwa kipindi cha wiki mbili kuazia siku ya Jumatatu wiki ijayo hadi kilio chao kitakaposikilizwa na washikadau wanaohusika.