array(0) { } Radio Maisha | Familia, Bungoma yalazimika kufukua mwili kufuatia mkanganyiko

Familia, Bungoma yalazimika kufukua mwili kufuatia mkanganyiko

Familia, Bungoma yalazimika kufukua mwili kufuatia mkanganyiko

Familia moja kwenye Kijiji cha Mayanja Kaunti ya Bungoma imelazimika kuufukua mwili waliouzika siku ya Jumamosi baada ya kuibuka madai kuwa walizika mwili usio wa jamaa wao.

Linah Bakari ambaye ni shangazi wa marehemu amesema huenda mkanganyiko huo ulisababishwa na kufanana majina ya marehemu katika hifadhi ya maiti

Inadaiwa familia hiyo iliuzika mwili wa mtoto Shantel badala ya mwanao Sharleen wote wakiwa wenye umri wa miaka miwili.

Kisa kingine cha kuzika maiti tofauti kilishuhudiwa wiki iliyopita eneo la Alupe Kaunti ya Busia baada ya familia moja kwenye Kijiji cha Kajoro Eneobunge la Nambale kuukosa mwili wa mmoja wao, uliokuwa umezikwa na familia nyingine.