array(0) { } Radio Maisha | Waziri wanne matatani kwa madai ya kumuua Naibu wa Rais Ruto.

Waziri wanne matatani kwa madai ya kumuua Naibu wa Rais Ruto.

Waziri wanne matatani kwa madai ya kumuua Naibu wa Rais Ruto.

Mawaziri wanne wa eneo la Mlima Kenya wamefika mbele ya Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi, DCI kurekodi taarifa kuhusu madai ya kupanga njama ya kumuua Naibu wa Rais William Ruto.

Aidha, mawaziri hao wanashutumiwa kwa kupanga mikutano kadhaa faraghani katika Mkahawa wa Lamanda wakijadili mbinu za kumzuia Ruto kutwaa wadhifa wa urais wakati Rais Uhuru Kenyatta atakapokamilisha hatamu za uongozi.

Inaarifiwa wanne hao ni Sicily Kariuki wa Afya, Joe Mucheru wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Peter Munya wa Viwanda na mwenzake wa Kilimo Mwangi Kiunjuri. Hata hivyo, Munya amesema kwamba hana kesi ya kujibu kwani hakuna mlalamishi na kuthibitisha kwamba wamekuwa wakikutana japo si kujadili masuala ya Ruto bali ya maendeleo ya eneo la Mlima Kenya.

Aidha, Munya amesema kwamba DCi wamewaelezea kwamba Ruto aliwasilisha rasmi malalamishi ya kuwepo kwa mikutano hiyo ya faragha akitoa mfano wa tarehe 14 mwezi Mei mwaka huu ambapo baadhi ya mawaziri hao walikutana katika Hoteli ya La Mada.

Hata hivyo Munya amesema hawatarekodi taarifa katika DCI hadi madai hayo yathibitishwe na mlalamishi ambaye ni Naibu wa Rais.