array(0) { } Radio Maisha | Mwanaume mmoja ajirusha ndani ya tanki Makueni.

Mwanaume mmoja ajirusha ndani ya tanki Makueni.

Mwanaume mmoja ajirusha ndani ya tanki Makueni.
Mwanaume mmoja amejaribu kujiua kwa kujirusha ndani ya tanki la maji eneo la Wote kaunti ya Makueni japo hakufariki dunia kwani tanki hilo halikuwa na maji.
 
Kulingana na Kamanda wa Polisi wa eneo la Makueni Timothy Maina, kisa hicho kiliripotiwa na wanakijiji cha Kaseve ambao walimpata jamaa huyo akiwa tayari amejitosa ndani ya tanki hilo kubwa.
 
Maafisa wa polisi walifika na kumwondoa ndani ya tanki hilo kabla ya kumpeleka katika Hospitali ya Makueni kwani alionekana kuwa alikuwa amedhoofika kiafya, na wakashuku huenda pia alikuwa amekunywa sumu.
 
Maafisa hao vilevile wamechukua simu aliyokuwa ameharibu pamoja na barua aliyokuwa amemwandikia dadake, mwanawe na mkewe akieleza sababu zake za kutaka kujiua.