array(0) { } Radio Maisha | Naibu wa Rais asisitiza kuwa ataendelea kutoa michango makanisani.

Naibu wa Rais asisitiza kuwa ataendelea kutoa michango makanisani.

Naibu wa Rais asisitiza kuwa ataendelea kutoa michango makanisani.

Naibu wa Rais William Ruto amesisitiza kwamba ataendelea kutoa michango makanisani licha ya Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa, John Mbadi kutishia kuwasilisha mswada ili kuhakikisha hakuna kiongozi anayetoa zaidi ya shilingi laki moja katika michango.

Akizungumza kwenye Kaunti ya Vihiga, Ruto aidha amesema makanisa mengi nchini yanapaswa kujengwa hivyo hatasita kuwasaidia viongozi wa makanisa iwapo ataombwa kufanya hivyo.

Ruto amewashauri wabunge kutojadili mswada huo na badala yake kuhakikisha miswada inayolenga kupiga jeki miradi ya maendeleo inapitishwa.

Ruto ameandamana na aliyekuwa Gavana wa kaunti hiyo, Moses Akaranga, wabunge Charles Gimose, Benjamin Washiali na aliyekuwa Seneta wa Kakamega Boni Khalwale miongoni mwa viongozi wengine.