array(0) { } Radio Maisha | Mwanaume wa miaka ishirini ajeruhiwa na fisi Kajiado.

Mwanaume wa miaka ishirini ajeruhiwa na fisi Kajiado.

Mwanaume wa miaka ishirini ajeruhiwa na fisi Kajiado.

Mwanaume wa miaka ishirini na sita anaendelea kutibiwa katika hospitali ya Rufaa ya Kajaido baaada ya kujeruhiwa na fisi. Julius Somoire alikuwa akiwalisha mifugo wake msituni wakati alipovamiwa na mnyama huyo. Amesema alifanikiwa kuokolewa na wapita njia japo amejeruhiwa vibaya katika seheme mbalimbali mwilini ikiwamo miguu na mikono.

Madaktari katika hospitali hiyo ya Kajiado wameema mwathiriwa ametibiwa na hali yake imeimarika.

Somoire sasa ametoa wito kwa serikali Kupitai Shirika la Uhifadhi wa Wanyama Pori KWS, kumfidia.

Hayo yanajiri huku wakazi wakitishia kuwaua wanyama pori ambao wamekuwa wakiwahangaisha Kajiado.