array(0) { } Radio Maisha | Mwanafunzi wa kidato cha nne atiwa mbaroni kwa madai ya mauaji.

Mwanafunzi wa kidato cha nne atiwa mbaroni kwa madai ya mauaji.

Mwanafunzi wa kidato cha nne atiwa mbaroni kwa madai ya mauaji.

Mwanafunzi wa kidato cha nne ametiwa mbaroni kwenye Kaunti ya Kakamega kufuatia madai ya kumuua kwa kumdunga kisu mwanafunzi wa darasa la nane.

Kamanda wa Polisi katika kaunti hiyo Benard Muli amesema mwanafunzi huyo alitekeleza kisa hicho baada ya mzozo kuibuka baina yao kuhusu mpenzi wa kiume.

Muli amesema uchunguzi umeanzishwa kufuatia tukio lenyewe.