array(0) { } Radio Maisha | Orodha ya wabunge ambao hawajawahi kutoa mchango Bungeni.

Orodha ya wabunge ambao hawajawahi kutoa mchango Bungeni.

Orodha ya wabunge ambao hawajawahi kutoa mchango Bungeni.

Jumla ya Wabunge kumi wa kiume wa Bunge la Kitaifa hawajawahi kutoa mchango wowote wakati wa vikao vya bunge tangu Septemba maka 2017 hadi Desemba mwaka jana.

Miongoni mwa wabunge hao ni Mbunge wa Emgwen Alex Kosgey, Mwenzake wa  Kapseret Oscar Sudi na  Charles Kamuren  wa Baringo Kusini. Wengine ni Samuel Arama  wa Nakuru mjini Magharibi, James Githua Wamacukuru wa Kabete, Justus Kizito wa Shinyalu, Alfred Sambu wa Webuye Mashariki na Joshua Adama wa Nyakach.

Ripot hiyo ambayo imetolewa leo hii na Shirika la Mzalendo Trust imemworodhesha Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichungwa kuwa miongoni mwa wanaoongoza kutoa michango bungeni. Wengine ni Mbunge wa Kipkelion Mashariki Joseph Kirui Limo na Robert Pukose wa Endebess.

Wengine wanaoongoza katika kujukumika vyema Bungeni ni Kiongozi wa Wengi Adan Duale, Mwenzake wa Wachache John Mbadi Vile vile Spika Justin Muturi.

Wawakilishi wa Kike watano miongoni wa Arubaini na saba hawajawahi kutoa mchango wowote. Wawakilishi hao nni 5 Anab Mohamed wa Garissa, Lilian Tomitom wa Pkot Magharibi, Irene Kasalu  wa Kitui, Jane Wanjuki wa Embu na  Jane Chebaibai wa Elgeyo Marakwet.

Kwa upande mwingine Sabina Chege wa Murang’a, Gladys Boss Shollei wa Uasin Gishu na Gladys Atieno   wa Homa Bay ni miongoni mwa wanaoongoza katika kutoa michango.

Katika Seneti wale wanaoongoza ni Johnson Sakaja wa Nairobi, Mutula Kilonzo Junior wa Makueni na Moses Wetangula wa Bungoma. Wengine ni  Anwar Loitiptip wa Lamu, Issa Juma Boy wa Kwale na Gideon Moi wa Baringo .