array(0) { } Radio Maisha | Wanawake wawili wakamatwa kwa kuwalaghai watu Kisauni.

Wanawake wawili wakamatwa kwa kuwalaghai watu Kisauni.

Wanawake wawili wakamatwa kwa kuwalaghai watu Kisauni.

Polisi eneo la Kisauni kwenye Kaunti ya Mombasa wamefanikiwa kuwakamata wanawake wawili ambao wamekuwa wakiwalaghai watu kwa kuwauzia kipande cha ardhi katika eneo la  Mwembelegeza. Inaarifiwa ardhi hiyo inamilikiwa na mtu  mwingine ambaye tayari amejenge kwenye ardhi hiyo.

Kamanda wa Polisi eneo la Kisauni Julius Kiragu amesema kwamba Mwanaisha Mwakirunga mwenye umri wa miaka 39 na mwenzake wamekuwa wakiwauzia watu hao kipande hicho chenye mita hamsini kwa mia.

Amesema kwamba polisi wamepata taarifa kuwahusu wawili hao kutoka kwa mtu ambaye walikuwa wamemuuzia kipande hicho kwa shilingi milioni 1.7 na tayari alikuwa amelipa shilingi milioni moja.

Mwanamme huyo amewaarifu polisi baada ya kuwaita wawili hao ili awalipe deni la shilingi laki saba ambazo alikuwa anadaiwa ndiposa wakamatwa.

Kiragu amedokeza kwamba mwanamme huyo na mtu mwingine ambaye pia alilaghaiwa shilingi laki tisa walipewa hatimiliki bandia zote zenye nambari zinazofanana.

Wanawake hao wanazuiliwa kwenye Kituo Cha Polisi cha Bamburi wakisubiri kufikishwa mahakamani kesho kufunguliwa mashtaka.