array(0) { } Radio Maisha | Gideon Moi atuma risala za rambi rambi kwa familia ya Benson Kiptire.

Gideon Moi atuma risala za rambi rambi kwa familia ya Benson Kiptire.

Gideon Moi atuma risala za rambi rambi kwa familia ya Benson Kiptire.

Mwenyekiti wa chama cha KANU , Gideon Moi amekuwa kiongozi wa hivi punde kutuma risala za rambi rambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwakilisi Wadi Benson Kiptire.

Moi amemtaja  Kiptire kuwa rafiki wa karibu  vilevile kuchangia maendeleo alipokuwa Mwakilishi Wadi wa eneo la Kipyego kupitia chama cha KANU.

Kiptire alikuwa Mwakilishi Wadi kati mwaka 2013 na 2017 kabla ya kuchaguliwa kuwa mmoja wa wasaidizi wa Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen. Kiptire alichukuliwa na watu waliojifanya kuwa maafisa wa polisi Ijumaa kabla ya mwili wake kupatikana kichakani katika  Kaunti ya Pokot Magharibi.  Mwili ulipatikana na majeraha ishara ya kuuliwa kwa kifaa butu. Hata hivyo uchunguzi umeanzishwa rasmi kufuatia kisa hicho.

Viongozi  kadhaa wa Elgeyo Marakjwet wanaendelea kuitembela familia hiyo katika eneo la Rock Center barabara ya Iten- Eldoret.