array(0) { } Radio Maisha | Mabalozi wa UAE kushirikiana na mbunge wa Saboti Caleb Amisi.

Mabalozi wa UAE kushirikiana na mbunge wa Saboti Caleb Amisi.

Mabalozi wa UAE kushirikiana na mbunge wa Saboti Caleb Amisi.

Mabalozi wa mataifa ya Saudia na wa Muungano wa Milki za Kiarabu UAE wameihakikishia serikaliya Kenya na uongozi wa Eneo Bunge la Saboti ushirikiano dhabiti kwa madhumuni ya kufanikisha miradi ya maendeleo pia kuboresha maisha  Wakenya wanaoishi kwenye maeneo ya mabanda.
 

Wakati wa kikao na wanahabari muda mfupi baada ya kuuzindua mpango wa kutoa msaada wa  chakula na bidhaa nyingine kwa wakazi zaidi ya elfu 10 katika mitaa hiyo ya mabanda Matisi na Kipsongo,  Balozi wa Taifa la Saudia nchini Mohamed Khayat na mwenzake  wa United Arap Emarates Khalid Khalifa al Mualla kwa pamoja wamekariri kuwekeza  katika sekta  elimu ili kuyasawazisha maisha ya watu wenye tabaka la juu la chini.

Kadhalika mbunge wa eneo hilo, Caleb Amisi amesema atajibidiisha kuboresha maisha ya wenyeji hao kwa kushirikiana na wafadhili mbalimbali.

Eneo Bunge la Saboti ni mojawapo ya maeneo bunge chache nchini yaliyo na mitaa ya mabanda ambayo wakazi wake wanaendeleo kuongezeka kila mwaka.