array(0) { } Radio Maisha | Walimu katika tasisi ya Utabibi kuongezewa mishahara.

Walimu katika tasisi ya Utabibi kuongezewa mishahara.

Walimu katika tasisi ya Utabibi kuongezewa mishahara.

Walimu wote wanaohudumu katika Tasisi ya Utabibu KMTC wataongezwa mishahara. Mwenyekiti wa Tasisi hiyo Profesa Philip Kaloki amesema kwamba hatua hiyo inafuatia Tasisi hiyo kupandishwa kiwango kutoka Level Two hadi Level Four.

Akizungumza Jijini Mombasa, Kaloki amesema kwamba walimu hao pia watakuwa wakipata marupurupu mbalimbali.

Kadhalika amesema kwamba Usimamizi wa Tasisi hiyo inaendeleza mazungumzo ya kufungua Vyuo vya KMTC kwenye Kaunti za Marsabit, Kirinyaga, Narok na Samburu.