array(0) { } Radio Maisha | Uchunguzi unaendelea kufuatia kifo cha Benson Kiptire.

Uchunguzi unaendelea kufuatia kifo cha Benson Kiptire.

Uchunguzi unaendelea kufuatia kifo cha Benson Kiptire.

Polisi wanaendeleza uchunguzi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwakilishi Wadi Benson Kiptire.

Kiptire ambaye alikuwa msaidizi wa Seneta wa Elgeyo Marakwet, Kipchumba Murkomen, alichukuliwa na watu wasiojulikana Ijumaa mchana mjini Eldoret kabla ya mwili wake kupatikana jana katika Kaunti ya Pokot Magharibi ukiwa na majeraha. 

Seneta  Kipchumba Murkomen amewataka wakenya kuwapa nafasi maafisa wa polisi kukamilisha uchunguzi.

Hayo yakijiri Gavana wa  Elgeyo Marakwet Alex Tolgos anatarajiwa kuongoza ujumbe wa viongozi kadhaa wa Elgeyo kuitembela familia ya mwendazake mjini Eldoret.