array(0) { } Radio Maisha | Wanakandarasi kupewa kipau mbele katika nafasi za uajiri kaunti Nairobi.

Wanakandarasi kupewa kipau mbele katika nafasi za uajiri kaunti Nairobi.

Wanakandarasi kupewa kipau mbele katika nafasi za uajiri kaunti Nairobi.

Serikali ya Kaunti ya Niarobi imetangaza kuwa itawaopa kipaumbele wafanyakazi wa kandarasi na wanaojitolea wakati nafasi za kazi zinapotokea. Gavana Mike Sonko ameiagiza Bodi ya Huduma za Umma ya Kaunti kuhakikisha kuwa wafanyakazi hao wanaajiriwa kwanza kabla ya kuzingatia wengine waliotuma maombi.

Sonko amesema serikali yake imebuni bodi itakayosimamia uajiri wa wafanyakazi na shughuli yenyewe itafanywa kwa haraka, vile vile kwa uwazi na haki.

Amesema sekta ya afya na elimu ya chekechea kwenye kaunti yake ina wafanyakazi wengi walioajiriwa kwa kandarasi huku akisema ndio watakaozingatiwa kwanza katika mpango huo.


Amesema kuna jumla ya shule mia mbili ishirini na tisa za chekechea zinazowahudumua wanafunzi elfu ishirini na moja.

Katika sekta ya afya kuna watu elfu sita wa kujitolea ambao wanahudumu aktika vituo vya afya hasa vilivyo katika mitaa ya babanda.

Kabla ya mwisho wa mwaka huu serikali ya kaunti ina mpango ya kutangaza nafas za kazi katika sekta hiyo ya afya.