array(0) { } Radio Maisha | Serikali kuu yatakiwa kusaidia kukailisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya kitale

Serikali kuu yatakiwa kusaidia kukailisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya kitale

Serikali kuu yatakiwa kusaidia kukailisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya kitale
Mwenyekiti wa Kamati ya Afya katika Seneti,  Michael Mbito ameirai serikali kuu kuiwezesha serikali ya Kaunti ya Trans Nzoia kifedha na vifaa vya matibabu kuikamilisha ujenzi wa Hospitali Level 6 unaoendelea.

Mbito ambaye pia ni seneta wa kaunti hiyo, amesema hospitali hiyo ni ya aina yake na  itakapokamilika itatoa huduma za afya sio tu kwa wakazi wa kaunti hiyo bali eneo la Magharibi ya Nchi, Kaunti za Pokot Magharibi, Turkana na Mashariki ya taifa la Uganda na lile la Sudan Kusini.

Kwa upande wake gavana wa kaunti hiyo, Patrick Khaemba amesema kufikia sasa serikali yake imezitumia shilingi milioni 800 kwa ujenzi wa hospitali hiyo na kwamba ili kukamilika  kinahitaji takribani shilingi bilioni 1.4.

Awali Naibu wa Rais, Daktari William Ruto alipoizuru kaunti hiyo alisema serikali kuu  imejitolea kuimarisha sekta ya afya na kuwa itashirikiana na uongozi wa kaunti hiyo kukamilisha mradi huo.