array(0) { } Radio Maisha | Gideon Moi afanya kikao na wakazi wa eneo la North Rift.

Gideon Moi afanya kikao na wakazi wa eneo la North Rift.

Gideon Moi afanya kikao na wakazi wa eneo la North Rift.

Seneta wa Baringo Gideon Moi amefanya kikao na wakazi pamoja na wazee wa eneo la North Rift wakati wa ziara yake ya siku mbili ili kutathmini maendeleo katika eneo la Bonde la Ufa.

Moi ambaye ameandamana a na viongozi wa kaunti za Pokot Magharibi, Elgeyo Marakawet na Baringo amesema kuna haja ya kutatua changamoto zinazowakabili wakazi.

Wakati wa mkutano na wakazi vile vile viongozi hao wamemtembelea Rais Mustaafu Daniel Arap Moi nyumbani kwake ambapo wazee wa Jamii ya Pokot wamemtawaza Moi kuwa kiongozi mwenye maono.

Miongoni mwa masuala ambayo yamejadiliwa wakati wa mkutano huo, ni kuhusu usalama vilevile miradi ya maendeleo.

Seneta moi amewahakikishia wakazi kwamba atazuru tena maeneo yao, ili kuendelea kushirikiana nao pamoja na viongozi kuhusu miradi ya maendeleo.