array(0) { } Radio Maisha | Maafisa zaidi watumwa kushika doria Yumbis.

Maafisa zaidi watumwa kushika doria Yumbis.

Maafisa zaidi watumwa kushika doria Yumbis.

Maafisa zaidi wa polisi wametumwa kwenye kaunti ay Garissa kuimarisha usalama kufuatia uvamizi uliotekelezwa katika kituo cha polisi cha Yumbis na washukiwa wa Al- shabaab. Msemaji wa Polisi Charles Owino aidha amewahakikishia wakazi usalama, huku akisema msako dhidi ya washukiwa zaidi unaendelea.

Awali katika taarifa kwa vyombo vya habari Owini alisema kwmaba polisi walifanikiwa kuwaua wahukiwa watatu wa uvamizi huo, huku wengine wakitoroka wakiwa na majeraha.

Washukia hao wanasemekana walitoweka na idadi isiyojulikana ya bunduki pamoja na risasi kutoka kituo hicho cha polisi kilichoko Eneo Bunge la Fafi, kilomita chache kutoka Somalia. Aidha waliharibu minara ya mawasiliano ya Safaricom.

Kisa hiki kimejiri wiki moja tu baada ya maafisa kumi na wawili wa polisi kufariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kukanyaga kilipuzi kilichokuwa kiemtegwa ardhini