array(0) { } Radio Maisha | Mudavadi amtaka Rais na kina wa Odn kukoma kuzungumzia handshake.

Mudavadi amtaka Rais na kina wa Odn kukoma kuzungumzia handshake.

Mudavadi amtaka Rais na kina wa Odn kukoma kuzungumzia handshake.

Kiongozi wa ANC, Musalia Mudavadi kwa mara nyingine amemtaka Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM Raila Odinga kukoma kulizungumzia suala la Handshake na badala yake kuwahudumia Wakenya.

Mudavadi amesema inasikitisha kuwaona viongozi hao wawili wakizungumzia jinsi walivyopatana ilhali Wakenya wanaendelea kuteseka. Amesema licha ya kutulia kwa joto la kisiasa nchini, Rais ameendelea kuzembea huku kauli zake za kulikabili jinamizi la ufisadi zikisalia kelele tu.

Akizungumza katika Shule ya Msingi ya Mbale alipoongoza hafla ya uzinduzi wa vitabu vya Maragoli ambavyo vitatumika kufanikisha Mtalaa wa Umilisi, CBC, Mudavadi aidha amempongeza amempongeza Gavana wa Benki Kuu, CBK Patrick Njoroge kufuatia kauli yake kwamba makataa ya kuzirejesha noti za shilingi elfu moja za zamani hayataongezwa.

Amesema kufikia sasa watu wengi waliopata mali yao kwa njia ya ufisadi wako kwenye njia panda kwani maelfu ya pesa zimewekwa majumbani na hata kwenye makontena katika benki za humu nchini na nje ya nchi.

Mudavadi aidha amewasihi Wakenya kuunga mkono vita dhidi ya ufisadi.