array(0) { } Radio Maisha | Ndege aina ya Cessna yalazimika kutua ghafla eneo la Molemu

Ndege aina ya Cessna yalazimika kutua ghafla eneo la Molemu

Ndege aina ya Cessna yalazimika kutua ghafla eneo la Molemu

Ndege aina ya Cessna imelazimika kutua ghafla eneo la Molemu kaunti ya Kwale baada ya kukumbwa ana hitilafu za kimitambo.

Ndege hiyo ilikuwa ikiondoka katika uwanja mdogo wa Chyulu kuelekea Diani wakati ilipotua.

Kamishna wa Kaunti ndogo ya Matuga  Isaac Keter amesema rubani wa ndege hiyo ambaye pia ni raia wa Afrika kusini amejeruhiwa.

Maafisa wa polisi na wale wa usimamizi wa viwanja vya ndege KAA na wazima moto wamefika eneo hilo na kuthibiti hali.

Hayo yanajiri huku ndege nyingine ya Shirika la Uhifadhi wa Wanyamapori KWS ikitua ghafla katika Mbuga ya Kitaifa ya Chyulu Kaunti ya Makueni. Polisi wamesema rubani yu salama.