array(0) { } Radio Maisha | maafisa wakuu wa utawadla kuhamishwa Pokot Magharibi.

maafisa wakuu wa utawadla kuhamishwa Pokot Magharibi.

maafisa wakuu wa utawadla kuhamishwa Pokot Magharibi.

Wizara ya usalama wa ndani imetakiwa kuwahamisha maafisa wakuu wa utawala wanaohudumu katika eneo la Pokot Magharibi kufuatia visa vya utovu wa usalama na mauaji ya mara kwa mara.

Kwa mujibu wa Mbunge wa Kapenguria, Samuel Moroto, licha ya kuwapo kwa maafisa wa usalama, baadhi ya wakazi wamekuwa wakiuliwa na watu wasiojulikana na kisha mili yao kutupwa.

Moroto amesema iwapo maafisa wa usalama wangekaza kamba basi visa vya utovu wa usalama havingeshuhudiwa kwani, sio jamii zote za eneo hilo zinajihusisha na visa hivyo bali sehemu ya watu fulani ambao wamekuwa wakitatiza usalama.

Kwa upande wake Mbunge wa Sigor, Peter Lokachapong amesema polisi wameshindwa kudhibiti mzozo miongoni mwa jamii za wafugaji eneo hilo kutokana na wizi wa mifugo unaoendelea kushuhudiwa.

Aidha ametaja hatua hiyo kuchangiwa na serikali kuwapokonya maafisa wa akiba, NPR bunduki ambapo imezifanya jamii kuzozana hata zaidi.

Hata hivyo aliposimama kuhutubia umma, kamishna wa eneo hilo amewashauri viongozi kukoma kuzungumzia matatizo yanayowakumba wenyeji hadharani na badala yake kuandaa mkutano ili kutafuta suluhu ya matatizo ya eneo hilo.