array(0) { } Radio Maisha | Mwanaume aliyemtishia Beatrice Ngatha maisha akamatwa na DCI.

Mwanaume aliyemtishia Beatrice Ngatha maisha akamatwa na DCI.

Mwanaume aliyemtishia Beatrice Ngatha maisha akamatwa na DCI.

Maafisa wa Idara ya Upelelezi, DCI wamenasa kadi hamsini na saba za simu kutoka kwa mwanamume aliyemtishia maisha   Beatrice Nkatha.

Polisi wamesema Joel Nyamio ambaye ndiye mshukiwa mkuu tayari anazuiliwa huku wakisubiri kufikishwa mahakamani Jumatatu.

Kwa mujibu wa DCI, kadi hizo zinajumuisha kumi na tisa za Kampuni ya Mawasiliano ya Safaricom, kumi na nane za Airtel na Telkom.

Mshukiwa huyo aliyekamatwa Ijumaa wiki hii aidha alinaswa na karatasi kadhaa zilizonakiliwa nambari za simu na majina ya wabunge kadhaa.