array(0) { } Radio Maisha | Gavana Alfred Mutua apinga wa kufunga baadhi ya mabewa ya vyuo vikuu

Gavana Alfred Mutua apinga wa kufunga baadhi ya mabewa ya vyuo vikuu

Gavana Alfred Mutua apinga wa kufunga baadhi ya mabewa ya vyuo vikuu

Gavana wa Machakos Alfred Mutua amepinga mpango wa Waziri wa Elimu George Magoha wa kufunga baadhi ya mabewa ya vyuo vikuu akisema Kenya inaviitaji hata zaidi.

Gavana Mutua anahofia mpango huo utarudisha nchi hii nyuma  akisema baada ya vyuo hivyo vikuu kufungua mabewa zaidi wanafunzi wamepata fursa ya kupata elimu ya juu bkwani idadi ya watahiniwa wanaohitimu kujiunga na vyuo vikuu nchini imekuwa ikiongezeka.

Gavana huyo aidha amesema vyuo hivyo vimewanufaisha zaidi wanafunzi wa mashinani ambao hukumbwa na matatizo ya kufika mijini ili kupata masomo yao.

Kauli yake Mutua inajiri kufuatia tangazo la Magoha la kuyafunga baadhi ya mabewa na akaonya wakuu wa vyuo hivyo dhidi ya kufungua vyuo zaidi.