array(0) { } Radio Maisha | Anaswa akiendesha shuguli ya kuavya mimba.

Anaswa akiendesha shuguli ya kuavya mimba.

Anaswa akiendesha shuguli ya kuavya mimba.

Maafisa wa Wizara ya Afya wa serikali kuu wakiwamo wa bodi ya wanafamasia, na wanachama wa bodi ya madaktari, KMPDU wamefanikiwa kumnasa mwanafunzi wa utabibu akiendesha shughuli za kuavya mimba.

Afisa wa KMPDU, Daktari Jonathan Buturu amesema kwamba msako wa kuzifunga vituo vya afya visivyozingatia sheria za utendakazi utaendelea kwa lengo la kuhakikisha kuwa Wakenya wanaotafuta huduma katika vituo hivyo hawaathiriwi. Kauli yake imetiliwa mkazo na Patrick Indika afisa wa bodi ya wanafamasia.

Luke Chemwolo ambaye ni afisa wa bodi ya maabara ameshangazwa kufahamu kwamba licha ya kuagiza kufungwa kwa kituo cha Sirikwa mwaka uliopita bado kilikuwa kinatoa hudumu bila kibali.

Mwaka uliopita maafisa wawili wa afya wafanyakazi wa serikali Kaunti ya Trans Nzoia walifikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kuendesha biashara ya maabara, kuuza na kutumia vifaa vya maabara kinyume na sheria.