array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta ashauri vyombo vya Habari vya kimataifa kuangazia mema Afrika.

Rais Kenyatta ashauri vyombo vya Habari vya kimataifa kuangazia mema Afrika.

Rais Kenyatta ashauri vyombo vya Habari vya kimataifa kuangazia mema Afrika.

Vyombo vya habari vya kimataifa vinapaswa kuangazia mema Barani Afrika wala si maovu kila wakati. Ndio kauli ya Rais Uhuru Kenyatta akiwahutubia maprofesa wa Chuo Kikuu cha Harvard katika Ikulu ya Nairobi.

Rais amesema vyombo hivyo vya habari vimesababisha bara hili kusalia nyuma kimaendeleo kufuatia taarifa zinazopeperushwa kuhusu Afrika. Amewashauri maprofesa hao kuwahamasisha wanahabari wa mataifa yaliostawi ili kuhakikisha mema yanaangaziwa.

Kwa upande wake Profesa Srikant Datar wa Harvard, amesema Afrika imepiga hatua kimaendeleo hivyo marais wa mataifa yaliostawi wanapaswa kuwarai raia wao kuwekeza katika bara hili.

Profesa Datar aidha amempongeza Rais Kenyatta kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha malengo yamaendeleo ya mwaka wa 2030 yanafaulu.

Wakati uo huo, Rais amesema bara hili limepiga hatua kisiasa kwani viongozi wanaendesha siasa za maendeleo badala ya zile za chuki. Amesifia mapatano kati yake na Kinara wa ODM Raila Odinga, akisema joto la kisiasa limetulia.