array(0) { } Radio Maisha | Msicahna wa miaka 21 auliwa kwenye kaun ya Makueni.

Msicahna wa miaka 21 auliwa kwenye kaun ya Makueni.

Msicahna wa miaka 21 auliwa kwenye kaun ya Makueni.

Familia moja  eneo la Mukaa Kaunti ya Makueni inaiomba serikali kuingilia kati ili haki itendeke kufuatia mauaji ya msichana wao wa miaka 21 ambaye alipigwa kwa kifaa butu kichwani vilevile kugongwa kwa nyundo tumboni ilhali alikuwa na ujauzito wa miezi sita.

Emily David alivamiwa na watu wasiojuliana tarehe 14 mwezi Juni akiwa katika chumba cha mpenzi wake walikokuwa wakiishi pamoja katika soko la Salama kisha kutendewa unyama huo.

Inaarifiwa Emily alimwita dadaye Josephine David saa chache baada ya uvamizi huo ambaye alimpeleka katika Hospitali ya Machakos Level Five ila akaaga dunia alipokuwa akitibiwa.

Babaye msichana huyo amesema kabla mwanawe kufariki, alilitaja jina la mpenziwe ishara tosha kwamba ni mhusika mkuu wa mauji hayo, hasa ikizingatiwa hakutaka mtoto aliyekuwa tumboni kuzaliwa.

Kamanda wa polisi wa Mukaa Benard Mugosho amesema kufikia sasa wamemkamata mpenzi wa msichana huyo na wanaendelea kumtafuta mwanamme mwingine ambaye anaaminika kutekeleza uvamizi huo.

Msichana huyo atazikwa nyumbani kwao leo huku familia yake ikiomba wote waliotekeleza kitendo hicho wakamatwe na kufunguliwa mashtaka ili haki ipatikane.