array(0) { } Radio Maisha | Mfutano kati wafugaji na wenyeji Taveta.

Mfutano kati wafugaji na wenyeji Taveta.

Mfutano kati wafugaji na wenyeji Taveta.
Wakazi kwenye eneo la Voi Kaunti ya Taita-Taveta wanaendelea kuwafurusha mamia ya ngamia wanaolishwa katika mashamba yao, licha ya kuwapo kwa makubaliano baina ya wafugaji na wamiliki wa mashamba.
 
Kulingana na mkataba uliotiwa saini  baina ya baadhi ya wamiliki wa mashamba hayo, ni kwamba wafugaji hao wanaruhusiwa kuwalisha ngamia wao, kwa miaka sita tangu Januari mwaka huu, hadi mwaka 2025.
 
Aidha mkataba huo unawataka wafugaji kulipia kima cha shilingi milioni 1.6 kila mwaka, kwa wamiliki wa mashamba hayo. Hata hivyo wafugaji wanalalamikia kuhangaishwa licha ya makubaliano hayo huku wakidai kwmaba suala hilo, limechochewa kisiasa na mmoja wa wanasiasa wa eneo hilo.
 
Ikumbukwe wiki chache zilizopita ngamia kadhaa waliuliwa huku mtu mmoja akijeruhiwa vibaya kufuatia kisa kinachoaminika kuwa cha ulipizaji kisasi.