array(0) { } Radio Maisha | Mbunge Moses Kuria asisitiza kufutiliwa mbali wadhifa wa Mwakilishi Wadi.

Mbunge Moses Kuria asisitiza kufutiliwa mbali wadhifa wa Mwakilishi Wadi.

Mbunge Moses Kuria asisitiza kufutiliwa mbali wadhifa wa Mwakilishi Wadi.
Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria amesisitiza kwamba wadhifa wa Mwakilishi wa Kike na ule wa Mwakilishi Wadi zinastahili kufutiliwa mbali ili kumpunguzia mzigo Mkenya mlipa-kodi.
 
Kuria ameliambia Jopo la Upatanishi, la Building the Bridges, BBI kwamba nyadhfa hizo mbili hazina maana hivyo zinapaswa kuondolewa kwenye mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho.
 
Hata hivyo Kuria amesema kwa sasa taifa haliko tayari kwa kura ya maamuzi kufuatia kupanda kwa gharama ya maisha hivyo shughuli ya kuifanyia katiba marekebisho iendeshwe bungeni na Wakenya kualikwa ili kutoa mapendekezo yao.