array(0) { } Radio Maisha | idadi ya walimu kuongezeka ili kuimarisha huduma kwa Waanafunzi.

idadi ya walimu kuongezeka ili kuimarisha huduma kwa Waanafunzi.

idadi ya walimu kuongezeka ili kuimarisha huduma kwa Waanafunzi.

Sekta ya elimu inaendelea kukua kila uchao huku serikali ikiwekeza pakubwa ili kufanikisha elimu miongoni mwa wanafunzi.

Akifungua rasmi Kongamano la Walimu katika eneo la Kabete-Kiambu, Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Huduma za Walimu, TSC Nancy Macharia aidha amesema idadi ya walimu imeongezeka ili kuhakikisha wanafunzi wanahudumiwa ipasavyo.

Kuhusu mishahara ya walimu, Macharia amesema serikali imetenga fedha nyingi kwa malipo ya walimu hao. Amesema fedha za kugharimia mishahara ya walimu zimeongezeka maradufu kati ya mwaka wa 2010 na 2019.

Wakati uo huo, Macharia amesema walimu zaidi wataajiriwa ili kufanikisha Mtalaa wa Umilisi, CBC.

Kongamano hilo limeanza mwendo wa saa tatu asubuhi huku likitarajiwa kukamilika kesho. Kaulimbiu mwaka huu ni Mwalimu Anayetoa Huduma za Mafunzo yenye ubora na Manufaa kwa Wanafunzi. Walimu na washikadau wataelezea changamoto zinazowakumba katika sekta hiyo vilevile hatua ambazo zimepigwa. Aidha walimu wamepewa fursa ya kuwatumbuiza wageni ambao wanahudhuria kongamano hilo