array(0) { } Radio Maisha | Makini Herbal yakanusha madai ya kufungwa.

Makini Herbal yakanusha madai ya kufungwa.

Makini Herbal yakanusha madai ya kufungwa.

Kliniki maarufu ya dawa za kinyeji Makini Herbal imekanusha taarifa kwamba kliniki hiyo imefungwa kufuatia msako ulioongozwa na Bodi ya Wanafamasia ya kuthibiti dawa na Sumu.

Akiongea na Radio Maisha kwa njia ya simu Daktari Wills Wanjala Wangwe amekiri kwamba maafisa wa Bodi hiyo walizuru kliniki yao jijini Nairobi japo hawakupatikana na hatia ya kukiuka kanuni za kuendesha biashara hiyo.

Aidha, Dkt Wanjala amethibitisha kwamba kliniki hiyo ingali inaendeleza shughuli zake kama kawaida.

Bodi hiyo ya Wanafamasia ilitoa taarifa ikisema kwamba Makini ilikuwa miongoni mwa kliniki 30 zilizofungwa kufuatia msako wao wiki hii. Aidha ilitaja kliniki za Murugu, Kamirithu, Olive herbal, East and West Medical Centre pamoja na klinki moja ya kichina iliyoko kwenye barabara ya Ngong jijini Nairobi kuwa zilizoathirika.

Maafisa wa Bodi hiyo walianzisha msako wa kliniki hizo zinazotoa dawa za asili ya kienyeji pamoja na dawa za kuuza dukani ambazo zimekuwa zikiendeshwa bila kuzingatia sheria ziliopo. Mmoja wa maafisa wa Bodi hiyo ya wanafamasia Dominic Kariuki ametaja msako huo kuwa ulizaa matunda na kwamba walipata dawa mbalimbali zinazotiliwa shaka ikiwemo za kupanga uzazi zilizokuwa na maandishi ya Kichina