array(0) { } Radio Maisha | Daktari amuagiza Mtoto kumdunga Mamaye.

Daktari amuagiza Mtoto kumdunga Mamaye.

Daktari amuagiza Mtoto kumdunga Mamaye.

Familia moja kwenye Kijiji cha Wamuini Eneo Bunge la Kiminini Kaunti ya Trans Nzoia imetoa wito kwa serikali kumchunguza dakatari ambaye anadaiwa kumpa maagizo mtoto wa umri wa miaka 16 kumdunga dawa mama yake akiwa nyumbani ambaye alikuwa akiugua maradhi ya kisukari.

Mtoto huyo ameiambia Radio Maisha kwamba muda mchache tu baada ya dadaye kumdunga mama yao dawa hizo kwa mujibu wa maagizo hayo ya daktari hali ya afya ya mamaye ikadorora hata zaidi.


Wanasema juhudi za kumsafirisha mama yao hadi Hospitali ya Level Four mjini Kitale ili atibiwe hazikufua dafu kwani kulingana naye alikuwa ameaga dunia tayari.

Mumewe marehemu amesisitiza haja ya uchunguzi wa kina kufanywa na daktari aliyetoa maagizo hayo kwa bintiye kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Usimamizi wa hospitali hiyo ambao haukutaka kurekodiwa umekisikitikia kisa hicho na kwamba tukio hilo halihusiani moja kwa moja na kituo hicho cha afya hasa ikizingatiwa kwamba mgonjwa huyo aliaga dunia akiwa nyumbani kwake.