array(0) { } Radio Maisha | Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuwasili mjini Eldoret.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuwasili mjini Eldoret.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuwasili mjini Eldoret.

Alasiri hii Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuwasili mjini Eldoret kwa ufunguzi rasmi wa kiwanda cha Rivatex, kilichofungwa  zaidi ya miaka kumi na mitano iliyopita. Rais Kenyatta ataandamana na Naibu Rais William Ruto.

Viongozi mbalimbali wamewasili mjini humo wakiongozwa na Waziri wa Viwanda Peter Munya kwa shughuli hiyo. Akizungumza mapema leo, Munya amesema kwamba tayari serikali imewewka mikakati kuimarisha uzalishaji katika kiwanda hicho. Miongoni mwa mikakati hiyo ni kusambaza mbegu ya zao la pamba lililobadilishwa kijenetiki yaani BT Cotton kwa wakulima ili kuhakikisha kwmaba kuna mali ghafi ya kutosha. Munya amesema ilivyo sasa amba inayozalishwa nchini haiwezi kutosheleza hitaji katika kiwnada hicho.

Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago, amesema huo utakuwa kwa manufaa sio tu kwa kaunti hiyo pekee  bali kwa kaunti jirani na wakazi. Amesema zaidi ya watu elfu kumi wataajiriwa kufuatia ufunguzi huo vile vile zaidi ya wakulima elfu kumi wa pembe wakitarajiwa kunufaika.

Mandago amesema wakulima wa zao hilo la pamba wamehangaika kwa muda mrefu kutokana na ukosefu wa soko na anatarajia kwamba baada ya Rivatex kufunguliwa tena watanufaika hata zaidi.

Mandago aidha ameiomba serikali kuwekeza zaidi kifedha ili kuhakikisha kiwnada hicho kinajisimamia.

Kauli ya Mandago imesisitizwa na mwenzake wa Elgeyo Marakwet, huku akiwashauri wakazi wa maeneo yaliyo karibu na kiwanda hicho kurejelea kilimo cha pamba kwa manufaa yao.

Hayo yanajiri huku viongozi wa eneo hilo, wakiongozwa na Mbunge wa Paseret Osca Sudi wakisisitiza kwamba hafla ya leo si ya kisiasa wakisema ni kwa manufaa ya wakazi.