array(0) { } Radio Maisha | azua kioja baada ya kujaribu kumchukua mwanawe.

azua kioja baada ya kujaribu kumchukua mwanawe.

azua kioja baada ya kujaribu kumchukua mwanawe.

Mama ya msichana ambaye alilelewa na mmoja wa wasichana pacha wa Kaunti ya Kakamega amezua kioja baada ya kujaribu kumchukua mwanawe mapema leo na hivyo kuzua mvutano miongoni mwao.

 

Kioja kimezuka baada ya Angelina Omina, ambaye alikuwa ameandamana na maafisa wa polisi kumchukua mwanawe Mevis Imbaya, wakati jamaa wa wasichana pacha walikuwa wakijiandaa kwenda kukutana na Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya ofisini mwake.

Omina anawashutumu jamaa hao kwa kumshinikiza mwanawe kuendelea kuishi na Rosemary Onyango, mama ya pacha hao nyumbani kwao katika kijiji Fufural, Kaunti ndogo ya Likuyani.

Kisa hiki kinajiri siku chache tu baada ya ripoti ya uchunguzi wa DNA kubainisha kwamba pacha hao walitenganishwa wakati wa kuzaliwa kwao katika hospitali kuu ya Kakamega. Hata hivyo familia hizo mbili ziliwahutubia wanahabari muda mfupi baadae na kusisitiza kwa kauli moja kwamba hawataifungulia mashtaka hospitali hiyo kwa mkanganyiko huo.