array(0) { } Radio Maisha | wanachama wawili wa bodi ya usimamizi wa hospitali ya Nairobi wajiuzulu

wanachama wawili wa bodi ya usimamizi wa hospitali ya Nairobi wajiuzulu

wanachama wawili wa bodi ya usimamizi wa hospitali ya Nairobi wajiuzulu

Masaibu yanayozingira usimamizi wa Nairobi Hospital yanaendelea kujitokeza huku wanachama wawili wa bodi ya usimamizi wa hospitali hiyo wakijiuzulu licha ya kutoa sababu rasmi.

Wanabodi hao ambao walichaguliwa hivi majuzi, Jaji Joyce Aluoch na daktari Eric Kahugu wamejiuzulu siku kadhaa baada ya mkutano wa kila mwaka wa wamiliki hisa za hospitali hiyo.

Hata hivyo, mfanyabiashara Joseph Wathoa Kigwe amejitolea kujaza wadhifa huo. Masaibu ya usimamizi wa Nairobi Hospital yaliibuka baada ya ripoti ya uhasibu ya Kampuni ya Ernst & Young iliyofichua kwamba kumekuwepo na visa vya ukiukaji wa sheria za ununuzi wa mali ya umma yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 130.